Jamii FM

Tani 112,303 za korosho zauzwa minada 10

27 October 2026, 07:52

Ofisi za Bodi ya Korosho Tanzania kwa mwonekano wa nje (Picha na Musa Mtepa)

Zaidi ya tani 112,303 za korosho zimeuzwa katika minada 10 ndani ya wiki mbili, huku CBT ikiwataka wadau kusimamia ubora na kupambana na ununuzi holela wa korosho maarufu kama Kangomba

Na Musa Mtepa

Zaidi ya tani 112,303 za korosho zimeuzwa katika minada 10 iliyofanyika ndani ya wiki mbili tangu kuanza kwa msimu wa mauzo wa mwaka 2026/2027, huku bei ya juu ikifikia shilingi 3,430 na bei ya chini ikiwa shilingi 2,970 kwa kilogramu moja ya korosho daraja la kwanza.

Akizungumza Oktoba 26, 2026, kuhusu mwenendo wa minada hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Frances Alfred, amesema minada hiyo imeonesha mwitikio mzuri wa wanunuzi tangu kuanza kwa msimu wa mauzo.

Aidha, amesema hadi kufikia Oktoba 26, 2026, jumla ya kampuni 90 zilikuwa zimejisajili kwa ajili ya kununua korosho, ambapo kampuni 57 tayari zimeshiriki katika minada na kushinda zabuni, huku akiwataka wadau kuendelea kusimamia ubora wa zao hilo.

Sauti ya Frances Alfred, Mkurugenzi Mkuu wa CBT

Katika hatua nyingine, Francs amewaomba viongozi wa vijiji, kata, wilaya na mikoa kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na ununuzi wa korosho kinyume na utaratibu, maarufu kama Kangomba, ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Sauti ya Frances Alfred, Mkurugenzi Mkuu wa CBT

Sambamba na hilo, amevikumbusha vyama vikuu vya ushirika kuhakikisha vinawalipa wakulima fedha zao kwa kuzingatia bei iliyopatikana katika mnada husika na daraja la korosho walizouza, badala ya kutumia bei ya wastani katika malipo ya wakulima.

Sauti ya Frances Alfred, Mkurugenzi Mkuu wa CBT