Jamii FM
Jamii FM
22 October 2026, 18:46

Taraka zimekuwa zikishamiri kila inapofikia wakati wa mavuno ya zao la korosho ambapo familia nyingi zimekuwa zikinufaika na pesa kutokana na mauzo ya zao hilo, nini huleta mzozo?
Na Mwanaidi Kopakopa
Msimu wa korosho ni kipindi muhimu kiuchumi kwa wakulima na familia nyingi mkoani Mtwara ambapo katika baadhi ya familia hupata mapato ya kutosha kutokana na kilimo, Moja ya mambo ambayo yanaweza kutokea ni pamoja na changamoto zinazohusiana na matumizi ya fedha, majukumu ya kifamilia, maamuzi ya pamoja na mahusiano ya wanandoa.
Kipindi hiki kinalenga kuchunguza kwa nini baadhi ya wananchi wanaona kuwa migogoro ya ndoa hujitokeza au kuongezeka wakati wa msimu wa korosho, pamoja na kutafuta njia zinazoweza kusaidia wanandoa kutumia mapato yao kuimarisha familia.