FM Manyara

Tanesco Manyara  yatoa tahadhari ya mvua za el nino

25 September 2026, 6:44 pm

Afisa uhusiano kwa umma kutoka Tanesco  Mkoa wa Manyara (Picha na Marino kawishe)

Tanesco Manyara  imesema wameshaanza maandalizi ya kuhamisha baadhi ya miundo mbinu ya Tanesco ikiwemo nguzo za miti 

Na Marino kawishe

Shirika  la umeme Tanzania Tanesco mkoani Manyara limewata wananchi wa mkoa huo kutoa taarifa iwapo wataona au kubaini changamoto ya miundombinu ya umeme kuathiriwa na mvua zilizotabiriwa kuwa kubwa za el nino.

Akizungumza na Fm Manyara kwenye kipindi cha mseto wa Leo Afisa uhusiano kwa umma kutoka Tanesco  Mkoa wa Manyara  Samweli Mandare amesema wameshaanza maandalizi ya kuhamisha baadhi ya miundo mbinu ya Tanesco ikiwemo nguzo za miti  zilizochakaa kwa kubadilisha na kuweka nguzo mpya za zege.

Sauti ya Afisa uhusiano kwa umma kutoka Tanesco  Mkoa wa Manyara

Nae Mhandisi wa Shirika hilo  Jinati Ally amewataka wananchi kuacha kufanya shughuli za kiuchumi chini ya Nyaya za umeme zinazokatisha kwenye maeneo yao kwaikua  inapotokea hitilafu inaweza kusababisha vifo au madhara mengine.

Sauti ya Mhandisi wa Tanesco Manyara

Aidha Shirika la umeme Tanzania Tanesco mkoani Manyara limewahakikishia ushirikiano wa kutosha wananchi na kuahidi kutatua mara moja changamoto yoyote itakayojitokeza pindi  wananchi hao watakapopiga namba ya bure 180 ya Shirika hilo.

Picha ya Mhandisi kutoka Tanesco Manyara Jinati Ally (Picha na Marino kawishe)