FM Manyara
FM Manyara
24 July 2026, 7:56 pm

Mafunzo ya Huduma ya kwanza kwa Askari wa wanyama pori yaliyojumuisha Askari kutoka TANAPA, TAWA, BWMA, BABATI DC NA CCA zinazofanya shughuli za uhifadhi wa wanyama pori katika ushoroba wa kwakuchinja pamoja na mfumo wa ikolojia ya Tarangire-Manyara yamefungwa rasmi leo julai 24 mwaka 2026.
Na Marino Kawishe
Akifungua mafunzo hayo mgeni rasmi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati, Mkuu wa Idara ya Maendeleo January Bikubwa amewataka Askari waliohitimu mafunzo hayo kuendeleza kwa wengine ambao hawakupata fursa hiyo ili elimu waliolyopata isaidie Jamii inayozunguka Hifadhi.

Akisoma Risala fupi ya mafunzo ya huduma ya kwanza kwa mgeni Rasmi lucas Zebruna amesema mafunzo yalilenga kuwapa washiriki ujuzi wa huduma ya kwanza kwa majeruhi kabla yakufikishwa hospitalini.
Kwa upande wake Mtendaji mkuu wa Taasisi Chem Chem ambao ndio Wafadhili wa mafunzo hayo Clever Zulu amesema mpango wa Taasisi hiyo nikuhakikisha inakuwa namba moja kwa kutoa elimu ya uhifadhi kupitia jamii kwa Bara la Africa.

Mafunzo hayo ya siku nne yaliyoanza Julai 20 mwaka huu hadi julai 24 yamejumuisha zaidi ya Askari 48 huku wakufunzi wakiw no Askari wa kikosi cha Anga Nchini Marekani kupitia ubalozi wao hapa nchini.