FM Manyara
FM Manyara
27 July 2026, 8:04 pm

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara, Regina Ndege ametoa mifuko 100 ya saruji na kuahidi kutembelea daraja lililokatika kwa mvua zilizopita na linalounganisha kitongoji cha Waloa na Kijiji cha Mwikantsi katika kata ya Mamire Wilayani Babati Mkoani Manyara
Na Marino Kawishe
Akizungumza na Waamini wa Parokia ya Mt Karol Langwa Mamire kwenye jubilee ya miaka 25 ya kwaya hiyo Naibu waziri amesema atatembelea kuona athari zilizosababishwa na mvua zilizopita ambazo ziliharibu kivuko cha eneo hilo.
Aidha kwa upande wake Diwani wa kata ya Mamire Augustino Sosiya akimkaribisha Naibu waziri amegusia Umuhimu wa kivuko hicho na kuomba kiweze kufanyiwa matengezo ya haraka kabla ya mvua kuanza kunyesha tena ambapo kijiji Tayari kimetenga kiasi cha sh milion 5.