FM Manyara

Siku ya vipimo yaadhimishwa Manyara kwa utoaji elimu

20 May 2026, 5:38 pm

picha ya meneja wakala wa vipimo mkoa wa Manyara Denis Misango 

Leo ikiwa ni kilele cha siku ya vipimo duniani, wananchi mkoani Manyara wametakiwa kufahamu vipimo sahihi wanaponunua bidhaa za mchanga, mawe kokoto na pumba  ili kuepuka kununua bidhaa hizo zikiwa na ujazo usio sahihi.

Na Mzidalfa Zaid

Wito huo umetolewa na meneja wakala wa vipimo mkoa wa Manyara Denis Misango  wakati akiongea na fm Manyara amesema wamekuwa wakifanya ukaguzi kwa kupima malori yanayobeba bidhaa hizo na kufahamu yamebeba ujazo kiasi gani.

sauti ya meneja wakala wa vipimo mkoa wa Manyara Denis Misango

Amesema ili mwananchi afahamu kama lori limehakikiwa lazima liwe na stika kutoka wakala wa vipimo ambayo inakuwa inaonyesha ujazo wa bodi, ambapo amewaonya baadhi ya madereva wasio waaminifu ambao wamekuwa wakiwadanganya wananchi kwa kuandika ujazo usio sahihi kwenye gari tofauti na ujazo ulizojazwa katikagari hilo.