FM Manyara

Kambi ya Madaktari Bingwa wa afya ya kinywa na meno yaanza leo Manyara.

27 July 2026, 8:33 pm

Picha ya Daktari Bingwa wa Afya ya kinywa na meno

Huduma za Matibabu ya Afya ya kinywa na Meno zimeanza kutolewa leo  katika Kambi ya Madaktari bingwaaa kutoka hospital ya Rufaa  Mkoa wa Manyara na huduma hizo zitatolewa Hadi julai 30 mwaka huu .

Na Emmy Peter

Wito huo  umetolewa na Leo daktari kutoka kitengo Cha huduma ya kinywa na Meno kutoka katika hospitali ya Rufaa  Mkoa wa Manyara Athumani Yatera alipokuwa akizungumza na Fm Manyara amesema huduma hiyo inalenga kutatua changamoto ya kinywa na Meno kwa Wananchi wa manyara na mikoa ya jirani.

Sauti ya daktari kutoka kitengo Cha huduma ya kinywa na Meno

Aidha amesema kufungua jalada na kumuona Daktari itakuwa ni bure kwa wasio na bima ila watachangia gharama za matibabu kwa kufuata utaratibu wa hospitali.