FM Manyara
FM Manyara
16 September 2026, 3:52 pm

Jamii ya wafugaji katika Kijiji cha Kimotoro, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wamepata fursa za uwezeshaji kutoka kwa mdau wa maendeleo, Taiko Kulunju.
Na Mzidalfa Zaid
Wanawake kutoka jamii ya wafugaji katika Kijiji cha Kimotoro, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, wameanza kuboresha maisha yao kiuchumi baada ya kupata fursa za uwezeshaji kutoka kwa mdau wa maendeleo, Taiko Kulunju.
Uwezeshaji huo unalenga kuwawezesha wanawake hao kuongeza kipato kupitia shughuli za uzalishaji, ikiwemo ufugaji na biashara ndogo ndogo, huku wakijenga uwezo wa kujitegemea na kusaidia familia zao.
Kwa muda mrefu, wanawake katika jamii za wafugaji wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa mitaji, hali iliyokuwa ikikwamisha juhudi zao za kujikwamua kiuchumi.
Kupitia mpango huo, Taiko Kulunju amechangisha jumla ya shilingi milioni 17,227,000 pamoja na dume moja la ng’ombe, kwa ajili ya kuwawezesha wanawake hao.
Viongozi wa Serikali na Chama katika eneo hilo wameunga mkono jitihada hizo, wakieleza kuwa uwezeshaji wa wanawake ni sehemu muhimu ya kuimarisha uchumi wa familia na jamii kwa ujumla.
