FM Manyara

Zimamoto yatoa tahadhari ya mvua Manyara

April 18, 2024, 12:05 pm

Kamishna msaidizi Gilbert Mvungi

kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kuleta madhara katika maeneo mengi nchini wananchi wanaoishi mabondeni wametakiwa kuhama

Na Emmy peter

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kuendelea kuchukua Tahadhari kutokana na mvua  zinazoendelea kunyesha nchini kwa baadhi ya maeneo ambapo  barabara na madaraja  yanajaa maji katika maeneo wanayoshi.

wito huo umetolewa leo na Kamanda wa jeshi la zima moto na uwokoaji mkoa wa Manyara Kamishna msaidizi Gilbert Mvungi alipokuwa akiongea na fm Manyara, amesema kwa wananchi wa mkoa wa Manyara waliopo mabondeni  mvua zinaponyesha maji yanajikusanya katika maeneo yao ambapo  wanapaswa kuchukua tahadhari  ikiwemo kuondoka maeneo  waliopo au walipojenga.

Kamishna msaidizi wa zimamoto Gilbet Mvungi

Kamanda Mvungi amesema wazazi wanapaswa kuwaangalia watoto wao wanapopita katika madaraja kwakua kunamadaraja rasmi na madaraja ya siyo rasmi yaliyowekwa magogo na katika  kipindi hiki  chamvua kumekuwa na changamoto nyingi za madaraja kujaa maji.

Aidha, amesema jeshi la Zimamoto na uwokoajia mkoa wa Manyara linaendelea kutoa elimu katika vyombo mbali mbali vya habari ikiwemo katika radio,runinga magazeti na mitandao ya kijamii.