FM Manyara
FM Manyara
14 July 2026, 10:32 pm

Wafungwa waliopatiwa adhabu ya kifungo kisichozidi miaka minne wametakiwa kufuatilia haki yao ya kuomba kutumikia sehemu ya kifungo chao wakiwa nje kupitia huduma kwa jamii, endapo watatimiza vigezo na masharti yaliyowekwa kisheria.
Na Mzdalfa Zaid
Hayo yameelezwa na Afisa huduma za uangalizi mwandamizi Mkoa wa Manyara,Tumain Mosha, amesema huduma kwa jamii ni mfumo wa utekelezaji wa adhabu unaolenga kuwapa nafasi wafungwa wanaostahili kutumikia kifungo chao wakiwa katika jamii chini ya uangalizi badala ya kuendelea kukaa gerezani kwa kipindi chote cha kifungo.
Aidha, amesema moja ya sifa muhimu ni mfungwa awe amehukumiwa kifungo kisichozidi miaka minne, na akisisitiza kuwa kila maombi hufanyiwa tathmini kwa kuzingatia masharti ya sheria ya huduma kwa jamii kabla ya uamuzi kufanyika.