FM Manyara

Wananchi Mbulu wahimizwa kutunza miundombinu ya maji

16 July 2026, 6:19 pm

Picha ikionyesha wakimbiza mwenge wakionganisha maji

Serikali inaendelea kuwekeza katika miradi ya maji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji kwa urahisi, hatua itakayowawezesha kutumia muda mwingi kufanya shughuli za kiuchumi

Na Benny Akaro

kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru 2026, Wazo Mwang’onda ameshiriki zoezi la kumuunganishia mwananchi huduma ya maji safi nyumbani ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali za kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.

Zoezi hilo limefanyika katika Halmashauri ya Mji wa Mbulu, ambapo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru amemuunganisha rasmi mwananchi na huduma ya maji kama ishara ya uzinduzi wa huduma hiyo na kuhamasisha wananchi kuendelea kunufaika na mradi huo kusema serikali inaendelea kuwekeza katika miradi ya maji ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji kwa urahisi, hatua itakayowawezesha kutumia muda mwingi kufanya shughuli za kiuchumi badala ya kutumia muda mwingi kwenda mbali kuchota maji.

Sauti ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge

Aidha, amewahimiza wananchi kuendelea kulinda na kutumia miundombinu ya maji kwa uangalifu pamoja na kuhakikisha huduma hiyo inatumika kwa manufaa yaliyokusudiwa.