FM Manyara

Babati DC yafanya kongamano la wanawake kuelekea siku ya wanawake

3 March 2026, 9:10 pm

Picha ya afisa maendeleo halmashauri ya wilaya ya Babati January Bikubwa

Halmashauri ya wilaya ya Babati imefanya kongamano la Wanawake katika shule ya msingi Vilima vitatu lenye lengo la kujadiliana kuhusu masuala ya haki za wanawake na wasichana kuelekea siku ya wanawake.

Na Marino Kawishe

Akizungumza  baada yakukamilika kwa kongamano hilo afisa maendeleo halmashauri ya wilaya ya Babati January Bikubwa amesema mada zote zilizopangwa zimejadiliwa kikamilifu. 

Sauti ya afisa maendeleo halmashauri ya wilaya ya Babati January Bikubwa

Aidha Mwakilishi wa shirika la STC Tanzania Grace Swai ambaye amezungumzia Maada inayolenga wanawake na dira ya Taifa ifikapo 2050 amesema lazima malezi kwa vijana ni jambo lakuangaliwa na jamii yote ili kufikia malengo ya Dira hiyo.

Sauti ya Mwakilishi wa shirika la STC Tanzania Grace Swai
Picha ya Mwakilishi wa shirika la STC Tanzania Grace Swai

Naye mwanasheria kutoka Shirika la CSP Eliakim Warikoy akitoa maada kwenye Kongamano hilo amesema kuwa jamii inapaswa kuacha kuendeleza mila potofu ambazo zimekuwa kichocheo cha ukatili kwenywe baadhi ya maeneo hapa Mkoani Manyara. 

Sauti ya mwanasheria kutoka Shirika la CSP Eliakim Warikoy
Picha ya mwanasheria kutoka Shirika la CSP Eliakim Warikoy

Maadhimisho ya siku ya wanawake kiwilaya yanatarajiwa kufanyika March 6 mwaka huu katika uwanja wa mpira wa kijiji cha Nkaiti Katika kata ya Nkaiti kuanzia asubuhi hadi jioni.