FM Manyara
FM Manyara
13 August 2026, 4:52 pm

Jamii mkoani Manyara imetakiwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika inapobaini vitendo vya usafirishaji haramu wa binadamu, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika.
Na Mzidalfa Zaid
Wito huo umetolewa na Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu Makao Makuu Dodoma, Consolatha Tarimo, wakati akitoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kutambua na kupinga vitendo hivyo kupitia kipindi Cha mseto wa Leo kinachorushwa Fm Manyara radio.
Tarimo amesema ushirikiano wa wananchi ni muhimu katika kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu, pamoja na kuhakikisha waathirika wanapata msaada na ulinzi unaostahili.