FM Manyara
FM Manyara
6 September 2026, 9:11 am

Walimu na Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari za wilaya ya Babati wamepata elimu ya ya matunizi ya Nishati safi ya umeme kwenye Mapishi.
Na Mzidalfa Zaid
Elimu hiyo imetolewa na Afisa Uhusiano wa shirika la umeme Tanzania Tanesco mkoa wa Manyara Samuel Mandari na Afisa huduma kwa Wateja Amiry Ahmed ambayo imelenga Kuongeza ufahamu na kuhamasisha wananchi wa wilaya ya Babati Kutumia nishati safi ya Umeme Kupikia.
Elimu hiyo ya Nishati safi imeenda sambamba na elimu ya Ulinzi wa Miundombinu ya umeme na Usalama wa Watumiaji.
Kwa upande wake Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Queen Sendiga David Swai ameahidi kufikisha taarifa kwa Wazazi wake juu ya umuhimu wa nishati safi ya kupikia huku walimu nao wakiahidi kuhamia kwenye Nishati ya umeme kupikia.
Aidha Kampeni ya kuhamasisha matumizi ya Nishati safi ya Umeme ya PIKA KIJANJA PIKA KWA UMEME inayotekelezwa na Shirika la Umeme TANESCO MKOA WA MANYARA inaendelea kwenye Maeneo tofauti Ndani ya Mkoa wa Manyara.