FM Manyara
FM Manyara
25 September 2026, 6:28 pm

Kutokana na uwepo wa vitendo vingi vyaukatili wa kijinsia maafisa ustawi wa jamii mkoani manyara wametakiwa kuhakikishaa vitendo hivyo vinaibuliwa na kukomeshwa
Na Hawa Rashid
Maafisa ustawi waJamii mkoani Manyara wametakiwa kuhakikisha wanasimamia vizuri masuala ya ukatili wa kijinsia katika Jamii pamoja na suala la lishe katika Shule zote ili Watoto wapate chakula chakutosha na kuwataka wazazi kusimamia vizuri malezi ya watoto bila kumuamini mtu yeyote.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Afya mkoa wa Manyara Thomas Male wakati akimwakilisha Mganga Mkuu wa mkoa wa Manyara katika kikao cha utekelezaji wa program ya taifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (MMAM na kuwakutanisha maafisa ustawi wa jamii katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Manyara ambapo amewataka Maafisa ustawi wa jamii kutekeleza waliyokubaliana katika kikao hicho
Kwa upande wao Maafisa ustawi wa Jamii kutoka Halmashauri mbalimbali za mkoawa Manyara wamesema katika kikao hicho wameona kuna changamoto mbalimbali ikiwemo Watoto kuto kutoa taarifa za unyanyasaji wanaoupitia kwa wakati, wakiwa shuleni, njiani na nyumbani na kuhakikisha kila mtoto anapozaliwa anapata cheti cha kuzaliwa na kupatiwa jina pamoja na kuwataka wazazi kuhakikisha wanawanyonyesha watoto wao pindi wanapozaliwa na kuwapalishe bora
Nae Afisa mradi wa mradi wa Mtoto kwanza Agostino Balogho kutokashirika la COSITA amesema katika utekelezaji wa mradi huo wanashirikiana na Serikali katika utekelezaji wake kwa ngazi yajamii na wamefanya tathmini ya utekelekezaji wamradi huo ambao umeanza mwezi wanne hadi mwezi wa tisa na wamepata picha halisi ya utekelezaji wake kwa ngazi ya Halmashauri kupitia Maafisa Ustawi wa Jamii kwa waliyoyafanya
Aidha amewataka Maafisa ustawi wajamii kuwa wavumilivu katika utekelezaji wa mradi huo wa MMAM kuwa wavumilivu kwasababu mradi huo unahitaji rasilimali fedha nanyenzo zote za kukabiliana namaeneo hayo kwakua wanakutana nawatua mbao wamekata tamaa zamaisha na changamoto za afya ya akili pamoja nakutokukata tama na kuwashirikisha wadau wengine wa maendeleo ili kuhakikisha mtoto anakuwa nautimilifu wa akili.

picha ya washiriki wa kikao cha mpango wa utekelezaji wa programu ya taifa ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (MMAM)