FM Manyara
FM Manyara
1 October 2026, 4:40 pm

Shirika la umeme Tanzania TANESCO mkoa wa Manyara limewataka wananchi kuchukua tahadhari na kuepuka kupaki magari, pikipiki au kufanya shughuli zozote karibu na maeneo yenye transfoma za umeme, kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kuhatarisha usalama wa maisha na mali.
Na Mzidalfa Zaid
Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kuchukua tahadhari na kuepuka kupaki magari, pikipiki au kufanya shughuli zozote karibu na maeneo yenye transfoma za umeme.
Akizungumza na fm manyara, afisa uhusiano wa TANESCO mkoa wa manyara Samuel Mandari, amesema wananchi wanapaswa kuzingatia usalama wanapokuwa karibu na miundombinu ya umeme, ikiwemo transfoma, na kuepuka kufanya shughuli zinazoweza kusababisha madhara.
Aidha,baadhi ya waendesha pikipiki mkoani Manyara wameonekana kutofahanu kupaki chombo cha usafiri karibu na miundombinu ya umeme kuna madhara na wengine wakiwa wana uelewa huo.