FM Manyara

Taifa Gas yatoa ofa ya punguzo la bei kwa mtungi mkubwa na jiko la gesi

18 November 2026, 6:04 pm

Picha ya meneja  Mauzo wa Taifa Gas Kanda ya Kaskazini, Ramadhani Msika(kulia) na Afisa Mauzo wa Taifa Gas Mkoa wa Manyara Lauriana Kitali(kushoto)

Kampuni ya Taifa Gas imeweka ofa maalumu ya punguzo la bei ya mitungi ya gesi kuelekea mwisho wa mwaka, inayomuwezesha mteja mwenye mtungi mdogo uliokwisha gesi kuubadilisha na kupata mtungi mkubwa pamoja na jiko la gesi plate mbili lenye kioo kwa masharti ya ofa hiyo na kuwawezesha wateja wapya kupata ofa hiyo kwa bei nafuu ya shilini 135,000.

Na Mzidalfa Zaid

Kuelekea mwisho wa mwaka, Kampuni ya Taifa Gas imeweka ofa maalumu ya punguzo la bei ya mitungi ya gesi pamoja na jiko lenye plate mbili ili kuwarahisishia wateja kupata huduma hiyo kwa bei nafuu.

Akizungumza na FM Manyara Radio, meneja  Mauzo wa Taifa Gas Kanda ya Kaskazini, Ramadhani Msika, amesema ofa hiyo inalenga kuwasaidia wateja kupata mitungi mikubwa itakayowawezesha kutumia gesi kwa muda mrefu zaidi bila kulazimika kujaza mara kwa mara.

Sauti ya meneja  Mauzo wa Taifa Gas Kanda ya Kaskazini, Ramadhani Msika

Amesema ofa hiyo ni fursa kwa wateja wenye mitungi midogo iliyokwisha gesi kufika katika vituo vya huduma vya Taifa Gas ili kubadilisha mitungi yao na kupata seti ya mtungi mkubwa pamoja na jiko la gesi.

Kwa upande wake, Afisa Mauzo wa Taifa Gas Mkoa wa Manyara Lauriana Kitali, amesema wananchi mkoani humo wameonesha mwitikio mkubwa kwa ofa hiyo, ambapo ndani ya wiki moja zaidi ya wananchi 20 tayari wamenufaika na mpango huo.

Sauti ya Afisa Mauzo wa Taifa Gas Mkoa wa Manyara Lauriana Kitali,