FM Manyara

Kanda Saba za mahakama zakutana Babati katika bonanza

1 November 2026, 8:37 am

Picha ya baadhi ya watumishi wa mahakama kutoka kanda saba za mahakama

Watumishi wa mahakama kutoka kanda saba nchini wamekutana mkoani Manyara katika bonanza la michezo mbalimbali lililofanyika katika viwanja vya Tanzanite Kwaraa, mjini Babati, kwa lengo la kuimarisha mshikamano na kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Na Mzidalfa Zaid

Kanda Saba za mahakama zimekutana mkoani Manyara katika viwanja vya Tanzanite Kwaraa na kushiriki michezo mbalimbali.

Akizungumza katika bonanza hilo, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mbwana Kambangwa, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Martin Shigela, amesema mahakama zina mchango mkubwa katika jamii, hivyo shughuli za aina hiyo ni muhimu katika kuimarisha mahusiano na ushirikiano miongoni mwa watumishi wa taasisi hiyo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mbwana Kambangwa,
Picha ya Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mbwana Kambangwa,

Kwa upande wake, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kanda ya Manyara, Dkt. Adam Mambi, amesema bonanza hilo limewakutanisha watumishi kutoka kanda mbalimbali za mahakama nchini, zikiwemo Manyara, Shinyanga, Tabora, Dodoma, Moshi, Arusha na Singida.

Sauti ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kanda ya Manyara, Dkt. Adam Mambi,
Picha ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kanda ya Manyara, Dkt. Adam Mambi

Amesema lengo la bonanza hilo ni kuwawezesha watumishi hao kubadilishana uzoefu katika kazi zao, kuimarisha ushirikiano na kujenga mshikamano kupitia michezo mbalimbali.

Nao baadhi ya washiriki wa bonanza hilo kutoka Tabora wamesema kuwa michezo imekuwa fursa muhimu ya kukutana, kufahamiana na kuimarisha mahusiano baina yao.

Sauti ya mshiriki kutoka Tabora

Washiriki wengine kutoka Shinyanga wameelezea umuhimu wa kuendeleza shughuli hizo kwa manufaa ya watumishi na taasisi kwa ujumla.

Sauti ya mshiriki kutoka Shinyanga
Picha ya baadhi ya viongozi