FM Manyara

Serikali kuweka mikakati kupunguza vifo vya mama na mtoto

8 October 2026, 6:45 pm

Picha ya katibu tawala mkoa wa Manyara pamoja na wataalam wa afya

Serikali imewataka Waganga wakuu wa mikoa kuweka miakati ya kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kipindi chote cha ujauzito na baada ya kujifugua.

Na Emmy Peter

Waganga wakuu wa mikoa mitatu  ikiwemo Manyara, Dodoma na Singida wametakiwa kuhakikisha wanaweka mikakati madhubuti ya kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa ujauzito na kujifungua.

Katibu tawala mkoa wa Manyara  Mariamu Muhaji ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wa mwaka wa tathmini ya huduma  ya afya ya uzazi na mtoto kanda ya kati kilichofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Manyara,amesema serikali inaendelea kuweka mipango na mikakati mbalimbali ya kuboresha huduma za afya kwa mama na mtoto, ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za kudhibiti vifo vitokanavyo na uzazi.

Sauti ya Katibu tawala mkoa wa Manyara  Mariamu Muhaji

Kwa upande wao wanganga wakuu wa mikoa  walioshiriki  mkutano huo wamesema maboresho ya huduma za mama na mtoto yameendelea kufanyika katika mikoa  yao  ikiwemo upatikanaji wa vifaa tiba pamoja na kutoa elimu kwa wanawake wajawazito kuhusu umuhimu wa kujifungulia katika vituo vya afya ili kuhakikisha wanapata huduma inayotakiwa  na kupunguza hatari ya vifo.

Sauti ya waganga wakuu

Aidha, wauguzi walioshiriki kikao hicho wameishukuru serikali kwa kuandaa semina hiyo, wakisema imewapa fursa ya kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu mbalimbali za kuboresha huduma kwa mama na mtoto, hatua ambayo itasaidia kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi wawapo  kazini.

Sauti ya wauguzi