FM Manyara
FM Manyara
17 April 2026, 8:24 pm

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara kupitia katibu Tawala msaidizi rasilimali Dominic Mbwete, amesitisha mnada wa mali za umma zilizokuwa zimetangazwa kuuzwa katika mnada kutokana na kuibuka sintofahamu kutoka kwa wafanyabiashara waliohudhuria kwa ajili ya kununua mali hizo.
Na Mzidalfa Zaid
Akiongea baada ya wafanyabiashara hao kulalamika, Mbwete amesema wameamua kusitisha mnada huo hadi April 18 2026 ili changamoto hiyo kutatuliwa na kutolewa tamko rasmi.

Kwa upande wao wafanyabiashara ambao wametoka maeneo tofauti hapa nchini wamesema mnada ulikuwa unafanyika kwa kinyume na taratibu ambapo wameishukuru serikali ya mkoa wa manyara kwa kuingilia kati mgogoro huo.
