FM Manyara

EWURA kanda ya kaskazini yakaribisha Wawekezaji kajenga vituo vya mafuta vijijini

10 August 2026, 11:51 am

Picha ya meneja Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini George Mhina (upande wa kulia mwenye miwani) akizungumza na Mwananchi aliyetembelea banda la EWURA katika viwanja vya Nane nane Njiro Jijini Arusha

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Kanda ya Kaskazini EWURA imewataka wananchi kuchangamkia fursa za uwekezaji kwakufungua vituo vya mafuta huku mamlaka hiyo ikiwahakikishia kuwa mamlaka inasimamia utoaji wa vibali na leseni za ujenzi na uendeshaji kwa kuzingatia sheria na viwango vya usalama.

Na Marino Kawishe

Akizungumza na Fm Manyara kutoka viwanja vya Nane nane Njiro Jijini Arusha Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini George Mhina amesema ili kuanzisha au kuwekeza kwenye kituo cha mafuta nchini  Tanzania kunahitaji kufuata hatua na masharti yaliyowekwa na mamlaka husika.

Sauti ya Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini George Mhina

Aidha amesema masharti hayo ni pamoja na umiliki wa eneo likiwa na Hati miliki au kibali halali cha matumizi ya ardhi kwa eneo linalokusudiwa, pamoja na Tathimini ya Mazingira ambapo utakuwa nanyaraka ya cheti cha mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC).

Picha ya Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini George Mhina akiwa pamoja na Afisa Uhusiano Mkuu wa wa EWURA Pamela Pallangyo wakiwa kwenye banda la EWURA katika maonyesho ya nane nane 2026 Njiro Jijini Arusha