FM Manyara

Manyara yajipanga kukabiliana na Elinino

15 September 2026, 11:47 pm

Picha ya mkuu wa mkoa wa Manyara Martin Shigela

Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na kamati mbalimbali za maafa wamejipanga kukabiiliana na athari za mvua Elinino zilizotabiriwa.

Na Emmy Peter

Mkoa wa Manyara umejipanga kukabiliana na madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño, huku kamati mbalimbali zikiandaliwa na kuwekwa katika utayari wa kuchukua hatua endapo mvua hizo zitasababisha athari kwa wananchi na miundombinu.

Akizungumza katika kikao Cha maandalizi hayo, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Martine Shigela, amesema mkoa umeweka mikakati na kuandaa kamati zitakazoshughulikia majanga, ikiwemo kuratibu hatua za uokoaji na kuwasaidia wananchi watakaoweza kuathirika.

Aidha, Lusungu Mwilongo, Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Mipango na Uratibu, amesema wamejipanga zaidi katika maeneo na wilaya ambazo zinaweza kuwa katika hatari kubwa ya kuathiriwa na mvua hizo ambapo

Amesema wananchi wanaoishi katika maeneo korofi wametakiwa kuwa kuhama kufuatilia taarifa za mamlaka ya hali ya hewa na kuchukua tahadhari mapema ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.

Sauti ya Lusungu Mwilongo, Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Mipango na Uratibu,
Picha ya Lusungu Mwilongo, Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Mipango na Uratibu

Naye Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati, Remidius Mwema, amesema wilaya zote za Mkoa wa Manyara wameweka Mikakati mbalimbali ya kukabiliana na madhara ya mvua hizo, ikiwemo maandalizi ya vikosi na kamati zinazohusika na kukabiliana na majanga ya Maji katika wilaya zenye changamoto za Mito Mikubwa na Mikondo ya Maji.

Sauti ya Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati, Remidius Mwema,
Picha ya baadhi ya washiriki