FM Manyara
FM Manyara
6 October 2026, 9:31 pm

Serikali mkoani Manyara imewataka wawekezaji kuwekeza ndani ya mkoa wa Manyara kutokana na fursa zinazopatikana katika mkoa huo.
Na Mzidalfa Zaid
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Martin Shigela, amewataka wawekezaji kuchangamkia fursa mbalimbali za uwekezaji zinazopatikana mkoani humo, akisema Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano na msaada unaohitajika katika shughuli za kibiashara na uwekezaji.
Shigela amesema Manyara ina fursa nyingi za uwekezaji katika maeneo mbalimbali hivyo wawekezaji wanapaswa kuzitumia fursa hizo kwa ajili ya kukuza biashara na kuchangia maendeleo ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake afisa Biashara mkoa wa Manyara Ally Mokiwa amesema Baraza la Biashara ni sehemu muhimu inayowakutanisha wafanyabiashara, sekta binafsi na serikali, kwa lengo la kujadili na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara pamoja na kuweka mazingira bora ya biashara.

Amesema ushirikiano huo unalenga kujenga dira ya maendeleo kuelekea mwaka 2050, huku changamoto za wafanyabiashara zikiendelea kutatuliwa kupitia majadiliano kati ya serikali na sekta binafsi.
Aidha mmoja wa wafanyabiashara hao mkurugenzi wa MATI SUPER BRAND LTD David Mulokozi amesema wanatamani kuona mawazo ya kibiashara wanayowasilisha kupitia kituo cha PPP yakipewa kipaumbele kwa wawekezaji wa ndani pindi fursa za tenda zinapotangazwa
