FM Manyara
FM Manyara
28 September 2026, 7:53 pm

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya stendi ya zamani wilayani Babati katika kampeini ya Linda ushirika chagua uadilifu kupitia clinic ya ushirika
Na Mzidalfa Zaid
Tume ya maendeleo ya ushirika(TCDC) imeendelea kutekeleza kampeini ya Linda ushirika chagua uadilifu kupitia clinic ya ushirika ambayo kwa mkoa wa Manyara inatarajia kufanyika September 30 Hadi ijumàa October 2 mwaka huu katika viwanja vya stendi ya zamani.
Hayo yameelezwa Leo na naibu mrajis wa vyama vya ushirika kutoka tume ya maendeleo ya ushirika Consolata Kiluma ambapo amesema Lengo la clinic hii ni kusikiliza kero , ushauri,maoni Pamoja na utolewaji wa elimu kwa wanaushirika pamoja na wadau wote wa ushirika .
Kwa upande wake Mkuu wa Huduma za Sheria tume ya maendeleo ya ushirika Osca Ng’itu amesema watashirikiana na wadau wa haki ikiwemo Takukuru, Mahakama, polisi katika kutatua migogoro mbalimbali.
Nae mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Manyara Absalom cheliga amesema mkoa wa Manyara una vyama vingi vya ushirika na kutoa wito kwa wananchi wa Manyara kujitokeza kwa Wingi kwa siku hizo tatu ili kupata elimu mbalimbali inayohusu ushirika
