FM Manyara
FM Manyara
19 November 2026, 10:03 pm

Wananchi wa Mkoa wa Manyara wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha kwa kuhakikisha wanatunza usafi wa mazingira, pamoja na kujenga na kutunza vyoo katika hali ya usafi na kufunika mashimo ya vyoo ili kuzuia uchafuzi wa mazingira.
Na Emmy Peter
Serikali mkoani Manyara imewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya magonjwa ya mlipuko kwa kuzingatia kanuni zote za afya katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha .
Afisa Afya wa Mkoa wa Manyara, Sweteni Mwabulambo, amesema wananchi wanapaswa kuhakikisha vyoo vinatunzwa katika hali ya usafi na mashimo yake yanafunikwa vizuri ili kuzuia maji ya mvua kuingia ndani ya mashimo hayo, hali inayoweza kusababisha uchafu kumwagika na kusambaa katika mazingira ya makazi ya watu.
Mwabulambo amesema kuzingatia kanuni za usafi ni hatua muhimu katika kuzuia maambukizi ya magonjwa na kulinda afya za wananchi katika kipindi hiki cha mvua.