FM Manyara

RC Sendiga awaonya watumishi wanaosababisha migogoro

13 May 2026, 6:54 pm

picha ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga, amesema atawachukulia hatua ikiwemo kuwapeleka Mahakamani watumishi ambao wanasabisha migogoro ya ardhi katika eneo la Makatanini wilayani Babati mkoani Manyara.

Na Mzidalfa Zaid

Sendiga amesema hayo Leo katika kikao Cha Baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Babati,na kukemea vikali vitendo vya baadhi ya watumishi wa serikali wanaoshikilia viwanja na kuwambia wananchi vimechukuliwa kwa maslahi yao binafsi.

sauti ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga

Katika hatua nyingine Sendinga amelitaka Baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Babati kutoweka vikwazo kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza baada ya kufunguliwa kwa geti la Mamire .

sauti ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Babati Yona Wawo , amesema amesema Baraza la madiwani limepitisha na kukubali uwekezaji unaotarajiwa kufanywa na Shirika la NSSSF katika halmshauri ya mji wa Babati.

Picha ya mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Babati Yona Wawo