FM Manyara

CCM yawataka wananchi kujiandiksha kwenye daftari la mpiga kura

10 October 2024, 5:04 pm

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura zoezi ambalo litaaanza October 11 hadi October 20 mwaka huu.

Na Mzidalfa Zaid

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara kimewataka  wananchi wenye sifa na nia ya kugombea nafasi za uongozi wa Serikali za Mitaa kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi za uongozi wa serikali za mitaa.

Akiongea na wanahabari  kwenye ofisi za chama hicho, Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) Mkoa wa Manyara Peter Toima amesema chama hakitaangalia mtu au kazi hivyo kila mtu ana haki ya kugombea.

Sauti ya Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) Mkoa wa Manyara Peter Toima

Katika hatua nyingine Toima amewataka wananchi mkoani Manyara kujitokeza  kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ili washiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Sauti ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Mkoa wa Manyara Peter Toima

Aidha, amesema chama hicho hakitakwenda na viongozi wasiofaa ambao walioshindwa kutekeleza majukumu yao katika kipindi kilichopita nakusema wanaataka viongozi watakaotekeleza ilani za chama cha mapinduzi