FM Manyara

Manyara yatajwa kuwa na wagonjwa wa afya ya akili

10 October 2025, 10:15 pm

Picha ya baadhi ya washiriki wa maandamano katika kilele Cha siku ya afya ya akili duniani.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amesema Manyara ni sehemu moja wapo ambayo inakabiliwa kwa kiasi kikubwa na ugonjwa wa afya ya akili kwani matukio ya kikatili, kujidhuru na kudhuru wengine yamekithiri .

Na Mzidalfa Zaid

Sendiga amesema hayo leo katika kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya akili duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Manyara katika viwanja vya moteli papaa.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga

Amesema madhara hayo yamekuwa yakisababishwa na mawazo, matumizi makubwa ya madawa ya kulevya, ukatili wa kijinsia, kipato duni na ukosefu wa ajira, lishe duni, utapiamlo na udumavu licha ya kuwa ni mkoa unaozalisha kwa wingi mazao aina zote ya chakula.

Picha ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara

Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya afya ya akili ya Mirembe, Dkt. Paul Lawala amesema ni vyema kuhakikisha wenye maradhi hayo wanafikishwa mapeka katika Hospitali hiyo, huku akielezea namna walivyojipanga katika kuboresha huduma za afya ya akili katika Mikoa na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, Dkt. Yesige Mutajwa ameeleza athari za matatizo ya afya ya akili kwa jamii ikiweo mauaji.