FM Manyara
FM Manyara
13 July 2026, 7:24 pm

Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi katika mradi wa maji katika kata ya Engusero Kijiji Cha nchinila unaotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) katika Wilaya ya Kiteto, Mkoa wa Manyara.
Na Emmy Peter
Mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 1.6 umekaguliwa na kiongozi mkimbiza Mwenge kitaifa Wazo Michael Mwang’onda na kuridhishwa na Mradi huo na kuwekea jiwe la msingi ambapo hatua hiyo ni utekelezaji wa wa miradi ya kimaendeleo katika Mkoa wa Manyara katika Miradi ya kimaendeleo sekta ya Maji.
Mradi huo unatarajiwa kunufaisha wananchi zaidi ya 25,000 kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama, hatua itakayochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi pamoja na kuboresha afya za wakazi wa eneo hilo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru alisisitiza umuhimu wa kutunza miundombinu ya maji ili huduma hiyo iendelee kuwafikia wananchi kwa muda mrefu na kuleta manufaa yaliyokusudiwa.
Aidha Akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Manyara, James Kiona Omela, amesema mradi umefikia asilimia 75 ya utekelezaji na unaendelea vizuri kulingana na mpango uliowekwa. Amesema mradi huo ukikamilika
Kwa upande wao, wananchi wa eneo hilo wameushukuru Serikali kwa kutekeleza mradi huo, wakisema utakuwa suluhisho la changamoto ya ukosefu wa maji iliyodumu kwa muda mrefu ambapo Mradi huo utahudumia Vijiji 3 .
