FM Manyara
FM Manyara
10 October 2024, 12:47 pm

Baada ya mtoto Joeli Mariki kupatikana akiwa hai katika mlima kwaraa , mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amesema madaktari wanaendelea kumpatia matibabu na hali yake bado inaendelea kuimarika kwa kuhakikisha anakuwa chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya.
Na Angel Munuo
Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amefika katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara kumjulia hali mwanafunzi wa shule ya sekondari Bagara Joeli Mariki ambaye alipotea tangu september 14,2024 katika eneo la mlima Kwaraa wilayani Babati mkoani Manyara ambapo alikwenda katika ziara ya mafunzo ya vitendo akiwa na wenzake .
Sendiga ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika hospitali ya mkoa wa Manyara ambapo amesema madaktari wanaendelea kumpatia matibabu na hali yake bado inaendelea kuimarika kwa kuhakikisha anakuwa chini ya uangalizi wa wataalamu wa afya.
Kwa upande wao wazazi wa Joeli wamesema furaha yao ni baada ya kumpata mtoto wao akiwa hai na kuwashukuru watanzania kwa maombi na kuwapa ushirikiano kwa kuhakikisha joeli anapatikana.