FM Manyara

Wanafunzi 460 Mdori kunufaika na mradi wa miaka 4 wa Chem Chem

13 August 2026, 5:15 pm

Picha ya Mkurugenzi mkuu wa CHEMCHEM ASSOCIATION akiwa na afisa miradi ya jamii wa Taasisi hiyo pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Mdori

Taasisi ya Chem Chem imekabidhi darasa Moja lililofanyiwa Maboresho,mashine ya kudurufu na computer mpakato mbili kwa Uongozi wa Shule ya Msingi Mdori iliyopo katika Kata Ya Nkaiti Wilayani Babati mkoani Manyara.

Na Marino Kawishe

Akisoma taarifa ya mradi huo wa miaka minne kwa mgeni Rasmi katibu Tawala wilaya ya Babati  Tobias  Abwao, Mkuu wa Shule ya msingi Mdori John Bura amesema mradi huo umegharimu zaidi ya shilingi milion 23 ambapo utakuwa kila mwaka unatengeneza Darasa Moja mpaka kumalizika kwake.

Aidha Mgeni Rasmi kwenye Halfa hiyo katibu tawala wilaya ya Babati Thobias Abwao Ameutaka uongozi wa shule kulinda rasilimali hizo walizopewa na Taasisi ya Chem Chem ili zitume kwa lengo lilikusudiwa.

Sauti ya katibu tawala wilaya ya Babati Thobias Abwao

Kwa upande wake afisa mradi ya jamii kutoka Chem Chem Napendael Wazoel Amesema Lengo lao nikuisaidia Jamii kupitia uhifadhi ambao umeendelea kuwanufaisha Wananchi ambao wapo pembezoni mwa hifadhi na ushirikiano wao ndio umepelekea wawekezaji kufanya kazi bila kikwazo.

Sauti ya afisa mradi ya jamii kutoka Chem Chem Napendael Wazoel

Mradi huo utanufaisha wanafunzi 460 wanaosoma kwenye shule hiyo na utakamilika 2029.

Picha za baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa