FM Manyara
FM Manyara
24 August 2026, 7:27 pm

Zaidi ya watoto laki moja na Ishirini na 8 elfu wenye umri chini ya miaka kumi katika halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya polio itakayotolewa kuanzia August 27 hadi 30 mwaka huu 2026.
Na Marino Kawishe
Akizungumza na baadhi ya Viongozi maarufu kwenye jamii ikiwemo Viongozi wa dini, mila na watoa huduma ya afya ngazi ya jamii kaimu Mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Babati Benedict Ntabagi amewataka wazazi kutumia muda huo kuhakikisha wanawatoa watoto wote wenye umri tajwa kupata chanjo hiyo.
Aidha mganga mkuu halmashauri ya wilaya ya Babati Dr Madama Hosea amesema maandalizi yote yamekamilika na halmashauri ya wilaya ya Babati iko tayari kufika kwenye maeneo yote ya wilaya kwani timu ya kutoa huduma ya chanjo imejipanga kwa zoezi hilo.
Viongozi mashuhuri kutoka kwenye jamii wamesema wapo tayari kuhamisha jamii kushiriki kikamilifu kwenye zoezi hilo na wajitokeze kwa wingi kwani chanjo hiyo haina madhara.
