FM Manyara

Chanjo ya polio awamu ya pili yaanza kutolewa Manyara

29 September 2026, 5:50 pm

Picha ya afisa afya mkoa wa Manyara Suten Mwabulambo

Chanjo ya polio awamu ya pili kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 10 imeanza kutolewa leo mkoani Manyara, ikiwa na lengo la kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa polio unaoweza kusababisha ulemavu.

Na Mzidalfa Zaid

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kutoa ushirikiano kwa serikali kuhakikisha watoto wenye umri chini ya Miaka 10 wanapatiwa chanjo ya polio awamu ya pili .

Akizungumza na FM Manyara, Afisa Afya wa Mkoa wa Manyara, Suten Mwabulambo, amesema chanjo hiyo inatolewa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu pamoja na nyumba kwa nyumba, ambapo zoezi hilo linatarajiwa kuendelea hadi Oktoba 2 mwaka huu.

Sauti ya afisa afya mkoa wa Manyara Suten Mwabulambo

Aidha, Mwabulambo amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanapatiwa chanjo hiyo, akisisitiza kuwa ni hatua muhimu katika kuwalinda dhidi ya ugonjwa wa polio na madhara yake, ikiwemo ulemavu.