FM Manyara

Msafara wa twende Butima watoa madawati zaidi ya 100

8 October 2026, 8:55 pm

Picha ya upandaji miti

Msafara wa waendesha baiskeli wa Twende Butiama, unaotoka jijini Dar es Salaam kuelekea Butiama mkoani Mara, kwa ajili ya kumbukizi ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, umeendelea kutoa msaada kwa jamii katika maeneo mbalimbali unapopita.

Na Mzidalfa Zaid

Msafara wa waendesha baiskeli wa unaotoka jijini Dar es Salaam kuelekea Butiama mkoani Mara, umeendelea kutoa msaada kwa jamii katika maeneo mbalimbali unapopita.

Tuungane na mwandishi wetu Mzidalfa Zaid kwa taarifa Zaidi.

Sauti ya mwandishi

Kwa upande wake, Kaimu Msaidizi wa Vodacom Kanda ya Kaskazini, Andrew Temu, amesema Vodacom imekuwa ikifadhili msafara huo kwa miaka minne mfululizo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kusaidia jamii, na kwamba itaendelea kushirikiana na msafara huo ili kufikia jamii kwa wigo mpana zaidi.