FM Manyara
FM Manyara
9 October 2026, 7:09 pm

Benki ya CRDB imemtembelea mjasiriamali anayefanya biashara ya mgahawa mjini Babati mkoani Manyara na kumzawadia vitu mbalimbali kwa kutambua uaminifu wake katika kukopa na kurejesha mikopo kwa wakati.
Na Mzidalfa Zaid
Katika kilele Cha wiki ya huduma kwa wateja Leo bank ya CRDB imemtembelea mama lishe ambae ni mteja wa CRDB na kumpa zawadi mbalimbali.
Akizungumza baada ya kumtembelea mjasiriamali huyo, Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Babati, Gloria Sam, amesema hatua hiyo ni sehemu ya shughuli za kijamii zilizofanywa na benki hiyo katika kilele cha Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Amesema miongoni mwa zawadi alizopatiwa mjasiriamali huyo ni namba ya malipo ya kuskani kwa kutumia simu au kadi, hatua inayolenga kurahisisha huduma za malipo katika biashara yake.

Kwa upande wake mjasiriamali huyo ameishukuru Benki ya CRDB kwa kumtembelea katika eneo lake la biashara, na kusema kuwa kuwa mikopo anayopata kutoka benki hiyo imemsaidia kukuza biashara yake.
Baadhi ya wateja walifika katika mgahawa huo wameeleza kufurahishwa na mfumo huo wa malipo kwa njia ya kuskani na kutumia kadi, wakisema unarahisisha malipo na kutoa urahisi zaidi katika upatikanaji wa huduma tofauti na ilivyokuwa awali.
