FM Manyara

TFRA na TAHA Yawanoa Wakulima wa Vitunguu

4 November 2026, 10:42 am

Picha ya Meneja wa TFRA Kanda ya kaskazini

Wakulima 35 kutoka kikundi cha wakulima katika Kijiji cha Jabag, Kata ya Balai, Mang’ola, Wilaya ya Karatu wamepatiwa mafunzo kuhusu matumizi sahihi ya mbolea katika zao la vitunguu, kwa lengo la kuongeza tija na kupunguza gharama za uzalishaji.

Na Mzidalfa Zaid

Mafunzo hayo yamefanyika katika Ofisi ya Kijiji cha Jabag kwa ushirikiano kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) na Chama cha Wakulima wa Bustani Tanzania (TAHA).

Picha ya baadhi ya wakulima waliopata mafunzo

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Meneja wa TFRA Kanda ya Kaskazini, Gothard Liampawe, amewatahadharisha wakulima dhidi ya matumizi yasiyo sahihi ya mbolea, ikiwemo kutumia mifuko 12 hadi 15 kwa ekari moja bila kuzingatia mahitaji halisi ya zao na matokeo ya vipimo vya afya ya udongo.

Liampawe amesema wakulima wanapaswa kuchagua aina ya mbolea kwa kuzingatia mahitaji ya virutubisho vya zao la vitunguu badala ya kutumia mbolea kwa mazoea au kutokana na mapendeleo yao.

Sauti ya Meneja wa TFRA Kanda ya Kaskazini, Gothard Liampawe,

Baadhi ya wakulima wameelezea namna walivyopata elimu mbalimbali ikiwemo kupima afya ya udongo ili kubaini mahitaji ya virutubisho na kuweka kiwango sahihi cha matumizi ya mbolea.

Sauti ya wakulima
Picha ya baadhi wakulima pamoja na wataalam wa TFRA