FM Manyara

(NSSF) yashauri wananchi kujiunga mfuko wa hifadhi skimu

24 April 2026, 1:02 pm

Picha ya wa mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) Alexanda Joseph

Mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) mkoa wa Manyara imewashauri wananchi kujiunga na kuchangia (NSSF) kwa wale ambao wamejiajiri au sekta binafsi  kupitia mfuko hifadhi skimu yaani mpango maalum unaolenga kuwawezesha wananchi walioajiriwa kujiunga na kuchangai (NSSF)  kulingana na kipato chao.

Na Mzidalfa Zaid

Ushauri huo umetolewa leo na Meneja wa mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) Alexanda Joseph, wakati akiongea na fm Manyara, amesema mpango huo unawapa fursa wananchi waliojiajiri kujiunga na kuchangia (NSSF) kulingana na kipato chao.

Sauti ya Meneja wa mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) Alexanda Joseph

Amesema faida za kujiunga ni pamoja na kupata sehemu ya akiba kwa dharura, kuchukua michango yake endapo atasitisha uanachama, kupata fao la matibabu, uzazi pamoja na  msaada wa mazishi.

Aidha, amesema walengwa wa skimu hiyo ni pamoja na, wakulima, wafugaji, wavuvi, wachimbaji wadogo, wasanii,machinga, bodaboda,wafanyabiashara wadogo na makundi yote ya waliojiajiri.