FM Manyara

Jeshi la zimamoto na Uokoaji Babati latoa elimu ya utayari wa majanga Sokoni

19 June 2026, 5:10 pm

picha ya baadhi ya maaskari wa jeshi la zimamoto na uokoani wakiwa katika zoezi la utayari wakizima moto katika eneo la soko kuu la Babati

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Babati leo limefanya zoezi la kutoa elimu ya utayari wa kukabiliana na majanga katika Soko Kuu la Babati mkoani Manyara, ambapo katika zoezi hilo kumetumika tukio la moto wa mfano ulioanzishwa katika eneo la choo cha soko.

Na Mzidalfa Zaid

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Babati, Emmanuel Kibona, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha wananchi wanapata elimu sahihi ya namna ya kukabiliana na majanga ya moto pamoja na kutambua mazingira rafiki yanayoweza kusaidia shughuli za uokozi na uzimaji moto pale dharura inapotokea.

Amesema wakati wa zoezi hilo imebainika kuwa baadhi ya njia zinazopaswa kutumiwa na magari ya zimamoto kuingia katika soko hilo si salama kutokana na kuzibwa na shughuli mbalimbali za biashara, hali ambayo inaweza kuchelewesha huduma za uokozi wakati wa majanga. 

sauti ya Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Babati, Emmanuel Kibona
picha ya Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Babati, Emmanuel Kibona kulia

Kwa upande wao, viongozi wa Soko Kuu la Babati akiwemo mwenyekiti, katibu na wajumbe wa soko pamoja na wafanyabiashara, wamelishukuru Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kutoa elimu hiyo wakisema imewasaidia kuongeza uelewa kuhusu utayari wa kukabiliana na majanga na umuhimu wa kushirikiana na vyombo vya uokozi ili kulinda maisha na mali za wananchi.

sauti ya viongozi wa Soko Kuu la Babati akiwemo mwenyekiti, katibu na wajumbe wa soko pamoja na wafanyabiashara,
picha ya baadhi ya viongozi wa soko