FM Manyara
FM Manyara
8 August 2026, 4:26 pm

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, ameipongeza FM Manyara Radio kwa mchango wake katika kuhabarisha na kuelimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo.

Na Emmy Peter
RC Sendiga ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea banda la FM Manyara Radio katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane Temi Njiro, mkoani Arusha, na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kituo hicho.
Aidha, RC Sendiga amewakaribisha wananchi kushiriki katika Marathon ya Msaada kwa Watoto Njiti, inayotarajiwa kufanyika tarehe 22 Agosti mwaka huu.
Amesema marathon hiyo inalenga kuchangisha fedha pamoja na kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa kuwasaidia watoto wanaozaliwa njiti kupata huduma stahiki za afya na nafasi ya kukua wakiwa na afya bora.
