FM Manyara
FM Manyara
23 April 2026, 10:08 pm

Mkuu wa Wilaya ya Hanang Almishi Issa Hazali ameunga mkono kwa vitendo agenda ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ya matumizi ya nishati safi kupikia, kwa kununua jiko la umeme lenye Presha (Electrical Pressure Cooker)
Na Mzidalfa Zaid
Akikabidhiwa Jiko hilo kutoka kwa Meneja wa TANESCO Wilaya ya Hanang Nadhir Yusuph pamoja na Afisa Uhusiano TANESCO Mkoa wa wa Manyara Samuel Mandari Hazali amesema amefuatilia taarifa za ufanisi wa majiko hayo kuwa ni mzuri sana yanatumia gharama ndogo kupikia,Muda mfupi kuivisha chakula pia yanatunza usafi wa mazingira.
Amesema amepata jiko hilo la umeme na atashirikiana na TANESCO kuhamsisha wakazi wengine zaidi wa wilaya ya Hanang kutumia umeme kupikia.
Shirika la Umeme TANESCO linaendelea na kampeni maalum ya Uhamasishaji matumizi ya nishati safi ya umeme Wilayani Hanang Kampeni hii imepangwa Kufikia Taasisi mbalimbali, wafanyakazi,Wafanyabiasha ,Wakulima na wanafunzi wilayani humo.