FM Manyara
FM Manyara
23 June 2026, 10:29 pm

Zoezi la ubadilishaji wa mita za kisasa za umeme (Smart Meter) linaendelea katika Mkoa wa Manyara na sasa limeingia katika awamu ya pili ambapo linafanyika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Manyara kwa lengo la kuboresha huduma za umeme na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa matumizi ya nishati.
Na Mwandishi wetu
Akizungumza na fm Manyara afisa uhusiani wa shirika la umemee Tanesco mkoa wa Manyara Samuel Mandari ,amesema wananchi wameendelea kujitokeza na kutoa ushirikiano kwa mafundi wanaotekeleza zoezi hilo, huku wakieleza matarajio yao ya kupata huduma bora zaidi kupitia matumizi ya mita hizo za kisasa.
Aidha Mandari amewahimiza wananchi kuendelea kushirikiana na shirika hilo wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo ili kuhakikisha linafanyika kwa mafanikio na kukamilika kwa wakati .
