FM Manyara
FM Manyara
29 April 2026, 1:13 am

Na Marino Kawishe.
Jumla ya wanavikundi 56 kutoka kwenye vituo vya taarifa na maarifa katika kata ya Mamire na Murray Mkoani Manyara wametoa tathimini ya utekelezaji mradi uletao mabadiliko ambao unatekelezwa kwenye halmashauri 6 na mikoa mitatu hapa nchini.
Wakizungumza na Fm Manyara Radio Wawakilishi wa vikundi hivyo wamesema zipo changamoto kadhaa ambazo zimekwamisha kufikia lengo la mradi huo na moja wapo ikiwa ni elimu.

Kwa Upande wake Msimamizi wa mradi huo kutoka mtandao wa Jinsia Tanzania Catherine Kasimbazi amesema lengo la kuanzishwa kwa mradi huo ni kutambua na kuwawezesha kuinuka kiuchumi wakulima ambao wanafanya kazi na mtandao huo wa Jinsia hapa Tanzania
Warsha hiyo ya siku mbili imeanza April 28 na imehudhuriwa na maafisa mbali mbali wa serikali kutoka ngazi ya kijiji hadi halmashauri zilipo kata hizo.

Picha ya wanavikundi kutoka kwenye vituo vya taarifa na maarifa katika kata ya Mamire na Murray wakiwa katika Warsha ya kufanya tathmini