FM Manyara
FM Manyara
5 August 2026, 11:25 pm

Kampuni ya PASS Leasing Limited inayotoa mikopo ya vifaa vya kilimo Imekabidhi Trekta aina Holland kwa mkulima kutoka Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro lenye Thamani ya zaidi ya shilingi milion 70.
Na Marino Kawishe
Akikabidhi Trekta Hilo Mkuu wa Wilaya ya Rombo Raymond Mwangwala amesema Kampuni hiyo imeendelea kuwa msaada kwa wakulima mbali mbali Hapa Nchini na Kutekeleza kikamilifu sera ya Rais Samia Suluhu Hasan kwenye Dira ya Taifa 2050.
Kwa upande wake Mkulima huyo amesema Kupata Trekta hilo litamuwezesha kufanya shughuli za kilimo kikamilifu na kuishukuru Kampuni ya PASSLeasing kwa kuendelea kuwawezesha Wakulima.
Aidha Afisa Mkuu wa PASS Leasing Kanda ya Kaskazini Neema Nyangalamela amesema wakulima waendelee kuwaamini Kampuni hiyo kwani Mikopo ya kilimo bado ipo hata baada ya Maonesho ya 32 ya nane nane mwaka 2026.
Maonesho hayo yanaongozwa na kauli mbiu inayosema kuwa ” Tambua Soko : Ongeza Tija kutekeleza Dira 2050.
