FM Manyara

Wanafunzi 4,083 kufanya upimaji wa taifa darasa la nne Babati TC

6 October 2026, 12:33 am

Picha ya Mkuu wa Idara ya Elimu ya Msingi wa Halmashauri ya Mji Babati Simon R. Mumbee,

Jumla ya wanafunzi 4,083 katika Halmashauri ya Mji Babati wameanza kufanya Mtihani wa Upimaji wa Taifa wa Darasa la Nne (SFNA), unaofanyika kuanzia Oktoba 5 hadi 6, 2026.

Na Mzidalfa Zaid

wakati mtihani wa darasa la nne ukiwa unaendelea nchini ,Jumla ya wanafunzi 4,083 katika Halmashauri ya Mji Babati wameanza kufanya Mtihani

wa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Elimu ya Msingi wa Halmashauri ya Mji Babati, Bw. Simon R. Mumbee, wanafunzi hao ni wavulana 2,073 na wasichana 2,010.

Amesema jumla ya shule 49 za Halmashauri ya Mji Babati zinashiriki katika mtihani huo, ambapo shule 35 ni za Serikali na 14 ni za binafsi.

Ameeleza kuwa kati ya shule hizo, 36 zinafundisha kwa mfumo wa Kiswahili, zikiwemo shule 35 za Serikali na moja ya binafsi, huku shule 13 zikiwa za mfumo wa Kiingereza na zote ni za binafsi.

Mtihani huo unalenga kupima uelewa na uwezo wa wanafunzi wa Darasa la Nne katika masomo mbalimbali, pamoja na kutathmini kiwango cha ujifunzaji katika elimu ya msingi