FM Manyara
FM Manyara
18 November 2026, 4:40 pm

Wakulima mkoani Manyara wameshauriwa kupanda mazao mapema katika kipindi hiki ambacho mvua zimeanza kunyesha kufuatia utabiri wa hali ya hewa uliotabiriwa kuwa kutakuwa na mvua kubwa za El Nino, hivyo ni muhimu wakulima kutumia fursa hiyo kwa kupanda kwa wakati.
Na Mzidalfa Zaid
Serikali mkoani Manyara imewashauri wakulima mkani Manyara kupanda mazao yanayoendana na ukanda wao pamoja na kufuata ushauri unatolewa na wataalamu kilimo katika kipindi hiki ambacho mvua zimeanza kunyesha.
Wito huo umetolewa leo na Afisa Kilimo Mkoa wa Manyara, Samuel Dahaye, wakati akiongea na FM Manyara amewataka wakulima kufuata ushauri unaotolewa na wataalamu wa kilimo kuhusu aina ya mbegu bora, muda sahihi wa kupanda na matumizi sahihi ya mbolea ili kuongeza tija.
Aidha, amewasisitiza wakulima kutokupuuza taarifa za utabiri wa hali ya hewa na badala yake wazitumie kama mwongozo katika shughuli zao za kilimo.