FM Manyara
FM Manyara
18 October 2026, 12:09 am

Wananchi mkoani Manyara wamevutiwa na bidhaa mbalimbali zinazopatikana katika Maonyesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair 2026, zikiwemo mashine za masaji na vifaa tiba vinavyotangazwa kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali ya kiafya bila kutumia dawa.
Na Mzidalfa Zaid
Maonyesho ya Tanzanite Manyara trade fair uameendelea kupamba moto baadhi ya wananchi wengie kushangazwa na mashine za vifaa tiba ambavyo vimesaidia kuwaponhesha wagonjwa bila kutumia dawa.
FM Manyara imetembelea banda la kampuni ya Shimomo Singapore inayouza bidhaa hizo, ambapo baadhi ya wananchi waliofika katika banda hilo wamepata fursa ya kujaribu vifaa hivyo na kueleza kuvutiwa navyo.

Akizungumzia matumizi ya mashine hizo, mwakilishi wa kampuni hiyo, Ema John, amesema vifaa hivyo vimekuwa vikitumiwa na watu wenye changamoto mbalimbali za kiafya, zikiwemo zinazohusiana na kiharusi (stroke).
Aidha, amewahimiza wananchi kutembelea banda la kampuni hiyo katika Maonyesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair yanayoendelea katika viwanja vya Tanzanite Kwaraa, Babati, ili kujionea bidhaa hizo na kupata maelezo zaidi kuhusu matumizi yake.
