FM Manyara

Manyara kupambana na magonjwa yasiyoambukiza

12 November 2026, 8:27 pm

Picha ya Mratibu wa Magonjwa Yasiyoambukiza kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Pastor Mahendeka,

Wiki ya maadhimisho ya magonjwa yasiyo ambukiza ambayo imeanza Novemba 9 hadi 14 mwaka huu mkoani Manyara imeadhimishwa kwa kuhamasisha jamii mkoani Manyara kuweka utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara .

Na Marino Kawishe

Wananchi Mkoani Manyara wametakiwa kupima afya zao mara kwa mara ili kufahamu hali zao za kiafya, kubaini changamoto zinazowakabili na kupata matibabu stahiki kulingana na magonjwa wanayougua.

Wito huo umetolewa na Mratibu wa Magonjwa Yasiyoambukiza kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Pastor Mahendeka, wakati akitoa elimu kuhusu namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa hayo kupitia kipindi cha Mseto wa Leo kinachorushwa na FM Manyara Radio.

Sauti ya Mratibu wa Magonjwa Yasiyoambukiza kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Pastor Mahendeka,

Aidha, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na mratibu huyo, takribani asilimia 30 ya wananchi wanakabiliwa na magonjwa yasiyoambukiza, yakiwemo kisukari, shinikizo la juu la damu, kifafa pamoja na changamoto za afya ya akili.