FM Manyara
FM Manyara
29 October 2026, 6:13 pm

Fm Manyara radio imetembelea gereza la wilaya ya Babati na kutoa misaada kwa wafungwa ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka Saba toka kuanzishwa kwake.
Na Mzidalfa Zaid
Katika kuadhimisha miaka saba tangu kuanzishwa kwake, kituo cha redio cha FM Manyara kimetoa misaada mbalimbali kwa wafungwa wa Gereza la Wilaya ya Babati mkoani Manyara, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kurudisha fadhila kwa jamii.
Akizungumza baada ya kukabidhi misaada hiyo, Mkurugenzi wa FM Manyara Radio, Mary Lekule, amesema kuwa imekuwa ni desturi ya kituo hicho kurudisha fadhila kwa jamii kila mwaka ambapo katika maadhimisho ya mwaka huu, wameamua kuwatembelea wafungwa ili kuwapa faraja na kuwafanya wajisikie kuwa sehemu ya jamii.
Kwa upande wake, Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Babati, SSP Bakari Gosori Rashid, ameushukuru uongozi wa FM Manyara Radio kwa kuwatembelea wafungwa na kuwapatia misaada hiyo, kwani itasaidia kukidhi baadhi ya mahitaji yao muhimu.
