FM Manyara
FM Manyara
10 October 2026, 9:55 am

Wafugaji Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wameonyesha kufurahishwa na uamuzi wa serikali wa kufanya mabadiliko katika sheria ya wanyamapori na kuondoa utaifishaji wa mifugo ambayo imewaumiza kwa miaka mingi.
Na Mzidalfa Zaid
Wamezungumza katika mkutano wa Naibu waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki na mbunge wa jimbo la Simanjiro James Ole Milya alipofika Katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi wa kijiji cha Kimotoroko na kusikiliza mahitaji yao ikiwemo changamoto ya maji katika zahanati ya kijiji chao.
Wakiongea kwa niaba ya wananchi mwenyekiti wa Kijiji Cha Kimotorok Elias Pamelo pamoja na mkazi wa eneo hilo Sipeo Koromo wameipongeza serikali kwa hatua hiyo huku wakielezea changamoto hiyo ya maji.
Baada ya kupokea shukrani na changamoto zao, Naibu Waziri James Ole Milya akatoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja na kuwataka wananchi wa Simanjiro kuendelea kuwa na subira wakati serikali inaendelea kutatua changamoto zao na kuboresha huduma za kijamii.