FM Manyara

Chanjo ya polio awamu ya pili kuanza Septemba 29 Manyara

23 September 2026, 2:35 pm

Picha ya Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Halmashauri ya wilaya ya Babati Mkoani Manyara James Mleli,

Wazazi na walezi mkoani Manyara wenye watoto wa umri chini ya miaka kumi wametakiwa kuhakikisha watoto wao wanapata Chanjo ya Polio ya awamu ya pili.

Na Diana Dionis

Kampeni ya chanjo ya Polio awamu ya pili inatarajiwa kuanza Septemba 29 hadi oktoba 2 mwaka huu 2026 Mkoani Manyara, huku wazazi na walezi wakihimizwa kuhakikisha watoto wenye umri chini ya miaka 10 wanapata chanjo hiyo ili kuendelea kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Polio.

Akizungumza na Fm Manyara, Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Halmashauri ya wilaya ya Babati Mkoani Manyara James Mleli, amewataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano kwa wahudumu wa afya pindi zoezi hilo litakapoanza.

Sauti ya James Mleli

Aidha Mleli amesema chanjo hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuwalinda watoto dhidi ya polio, ugonjwa ambao unaweza kusababisha ulemavu wa kudumu, huku akiwataka wananchi kutopotoshwa na taarifa zisizo sahihi kuhusu chanjo hiyo.

Sauti ya James Mleli

Kampeni hiyo inatarajia kuanza septemba 29 hadi oktoba 2 mwaka huu 2026 Mkoani Manyara, na Halamashauri ya Wilaya ya Babati inatarajia kuchanja watoto 147,583 hivyo wazazi na walezi wamehimizwa kuwa tayari na kuhakikisha watoto wanaostahili kupata chanjo hiyo wanapatiwa kikamilifu.